Ecuador wapewa holidei kusherehekea ushindi katika Kombe la Dunia

Ni mara ya pili kwa Ecuador kufuzu kwa hatua ya mwondoano ya Kombe la Dunia baada ya kuingia hatua hiyo  kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Dismas Otuke
1 Min Read

Leo Ijumaa, Juni 26, imetangazwa kuwa siku ya mapumziko nchini Ecuador ili kusherehekea ushindi wa timu yao wa mabao 2-1 dhidi ya Ujarumani jana usiku. 

Ecuador iliibuka kidedea katika mechi hiyo ya kundi E, matokeo yaliyoisaidia kufuzu kwa raundi ya 32 bora katika Kombe la Dunia linaloendelea.

Rais wa nchi hiyo Daniel Noboa kupitia ujumbe wake wa X , amesema ushindi huo ni wa kihistoria na unaweka kando shutuma ambazo timu hiyo ilipata baada ya kushindwa na Ivory Coast bao moja kwa bila katika mchuano wa ufunguzi na kwenda sare tasa na limbukeni Curacao katika mechi ya pili.

Ecuador walifungwa bao la mapema na Ujerumani jana Alhamisi lakini wakajizatiti na kupata ushindi wa magoli 2-1 uwanjani New York.

Ni mara ya pili kwa Ecuador kufuzu kwa hatua ya mwondoano ya Kombe la Dunia baada ya  kuingia hatua hiyo  kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

 

Share This Article