Kombe la Dunia: Ghana waishika mateka Uingereza

Uigereza wanaongoza kundi hilo kwa alama 4 sawa na Ghana iliyo ya pili wakati Croatia ikiwa ya pili kwa pointi tatu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Black Stars ya Ghana ililazimisha sare tasa dhidi ya Three Lions ya Uingereza katika mechi ya kundi L iliyoandaliwa uwanjani Boston, Marekani Jumanne usiku.

Licha ya mashambulizi tele kutoka kwa Waingereza, Ghana chini ya kocha mpya Carlos Quieroz alijihami vikali na kupata sare ambayo inawahakikishia nafasi katika raundi ya 32 bora.

Ghana watahitimisha dhidi ya Croatia Jumapili hii.

Croatia walihitaji bao la dakika ya 54 lake Ante Budmir ili kuibwaga Panama katika mechi nyingine ya kundi L mapema Jumatano uwanjani Toronto, Canada.

Uigereza wanaongoza kundi hilo kwa alama 4 sawa na Ghana iliyo ya pili wakati Croatia ikiwa ya pili kwa pointi tatu.

Panama wanashika nanga pasi na alama.

Share This Article