Rais Tshisekedi kuzuru Ituri kukadiria vita dhidi ya Ebola

Tom Mathinji
1 Min Read
Felix Tshisekedi - Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi amesema atazuru eneo la Ituri kulikozuka Ebola ili kukadiria vita dhidi ya ugonjwa huo hatari.

“Nachukua fursa hii kutangaza kwamba nitazuru mkoa wa Ituri kukadiria hali ilivyo binafsi,” alisema kwenye mkutano wa pamoja wa wanahabari na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Kulingana na Tshesekedi, kwenye mkutano wake na Ndashimiye, walielezea kujitolea kwao kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya, wakati huu ambapo eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya Ebola.

Viongozi hao wawili walihudhuria mkutano wa kikosi kazi cha kitaifa cha kukabiliana na Ebola mjini Kinshasa, ambapo Tshisekedi alidokeza kuwa mkutano huo umetoa taswira kamili kuhusu chamko la ugonjwa huo na hatua zinazopigwa za kukabiliana na msambao wake.

Watu zaidi ya 1,000 wameambukizwa Ebola huku zaidi ya 200 wakifariki kutokana na ugonjwa huo nchini DRC.

TAGGED:
Share This Article