Mabingwa wa Ulaya Uhispania, watarejea uwanjani Jumapili usiku dhidi ya Saudi Arabia, kwa mechi ya kwanza ya siku ya 11 ya patashika ya Kombe la Dunia.
Uhispania watashuka uwanjani Merces Benz, kuanzia saa moja usiku Jumapili katika mechi ya kundi H, ambayo ni sharti washinde ili kufufua matumaini ya kufuzu kwa hatua ya 32 bora,hususan baada ya kulazimishwa kwenda sare kappa na limbukeni Cape Verde, katika mechi ya ufunguzi wiki jana.
Saudi Arabia pia walitoka sare ya bao moja na Uruguay katika mchuano wa ufunguzi.
Baadaye saa nne usiku Ubelgiji wanaowinda kombe la kwanza watakabiliana na Iran,katika mechi ya kundi G, timu zote zikiwa na alama moja .
Uruguay watamenyana na Cape Verde, kuanzia saa saba kisha Misri wahitimishe ratiba ya siku dhidi ya New Zealand saa kumi alfajiri.