FIFA World Cup: Mexico ni ya kwanza kufuzu awamu ya 32 bora

Bao la ushindi lilipachikwa kimiani na Luis Romo katika dakika ya 50.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waandalizi wenza wa kipute cha Kombe la Dunia Mexico, ndio timu ya kwanza kujikatia tiketi kwa raundi ya 32 bora.

Hii ni kufuatia ushindi wa timu hiyo bao moja kwa bila dhidi ya Korea Kusini mapema Ijumaa ugani Guadalajara.

Bao la ushindi lilipachikwa kimiani na Luis Romo katika dakika ya 50.

Ushindi huo umewawezesha Mexico, maarufu El Tri, kuongoza kundi A kwa alama 6 na watakamilisha ratiba Jumanne ijayo dhidi ya Czechia.

Share This Article