FIFA World Cup: Raundi ya pili ya mechi za makundi kuanza leo

Saa kumi alfajiri, itakuwa zamu ya waandalizi wengine Mexico kukabiliana na Korea Kusini katika kundi A.

Dismas Otuke
1 Min Read

Raundi ya pili hatua ya makundi kuwania Kombe la Dunia itaanza leo Alhamisi kwa makundi ya A na B, katika siku ya saba ya kipute hicho.

Bafana Bafana ya Afrika Kusini, waliopoteza mchuano wa kwanza dhidi ya Mexico, watafungua mzunguko wa pili dhidi ya Czechia kundini A katika uwanja wa Mercede Benz nchini Marekani kuanzia saa moja.

Bosnia Herzegovina na Uswizi watashuka uwanjani Los Angeles kuanzia saa nne katika kundi B.

Wenyeji wenza Canada watakuwa  Vancouver saa saba usiku wa manane katika kundi B dhidi ya Qatar, huku mshindi akifufua matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mwondoano.

Saa kumi alfajiri itakuwa zamu ya waandalizi wengine Mexico kukabiliana na Korea Kusini katika kundi A.

Share This Article