Fainali za Kombe la Dunia za 23 zinaanza leo Alhamisi saa nne usiku kwa mechi ya ufunguzi kati ya Mexico na Afrika Kusini.
Kipute hicho kinashirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza kutoka32 za awali, na kitafanyika kati ya leo na tarehe 19 mwezi ujao katika mataifa ya Mexico, Canada na Marekani.
Kwa jumla, kati ya makala 22 yaliyopita ya Kombe la Dunia, nchi 8 zimeibuka mabingwa.
Timu tano za Ulaya zimenyakua kombe hilo mara 12 kwa jumla, huku timu 3 za Amerika Kusini zikitwaa ubingwa mara 10 kwa jumla.

Brazil imeshinda Kombe la Dunia mara tano, Uruguay mara mbili nao Argentina wakishinda mara mbili.
Katika kipute cha mwaka huu, Afrika inawakilishwa na timu 10, Asia 9, Ulaya 16, Amerika Kusini 6, Amerika Kaskazini 6 na Oceania 1.
Argentina ndio mabingwa watatezi baada ya kuishinda Ufaransa kupitia penalti katika makala ya mwaka 2022 nchini Qatar.