Kenya imedhamiria kuunga mkono mageuzi ya Shirika la Umoja wa Mataifa, UN kwa lengo la kuliwezesha shirika hilo kukabiliana na changamoto za karne ya 21 zinazoikumba dunia.
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki pia ameahidi kuwa nchi hii imekusuadia kuzungatia maadili ya UN.
“Kenya imekusudia kutilia maanani maadili na kanuni za UN, kuunga mkono mageuzi ya kuifanyia mabadiliko UN ili kuwa ya kisasa zaidi na taasisi yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za karne ya 21 zinazoikabili dunia,” alisema Prof. Kindiki.
Aliyasema hayo alipofanya mazungumzo na Rais wa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock afisini mwake katika jumba la Harambee House Annex, jijini Nairobi.
Naibu Rais akitumia fursa hiyo kuishukuru UN kwa kuweka makao makuu ya mashirika yake mawili ya UN na UN Habitat jijini Nairobi.
Aidha, aliishukuru UN kwa kuhamisha shughuli za mashirika ya UNICEF, UNFPA na UN Women kutoka jijini New York hadi Nairobi.
Waliokuwapo wakati wa mkutano huo ni Zainab Bangura (Mkurugenzi Mkuu wa UNON), Susan Nakhumicha (Mwakilishi wa
Kudumu wa Kenya katika UN-Habitat ) na maafisa waandamizi wa UN miongoni mwa wengine.
