Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imesema ilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa kusudi la kujibu shambulizi la awali ambapo helikopta ya jeshi la Marekani iliangushwa.
Kwenye ujumbe katika mitandao ya kijamii jana Jumanne, CENTCOM ilisema hatua hiyo ni “mwitikio mwafaka wa uchokozi usio halali wa Iran.”
Afisa mmoja wa Marekani alinukuliwa akisema mashambulizi hayo yalilenga mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran na rada iliyo karibu na Mlango Bahari wa Hormuz.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Iran ilidungua helikopta ya Apache wakati ikishika doria karibu mlango bahari huo.
Huku akisema marubani wawili waliokuwa kwenye helikopta hiyo wako salama, Trump alitoa onyo kali kwamba Marekani sharti ijibu” shambulizi hilo.
Kwa mujibu wa CENTCOM, helikopta hiyo ilianguka karibu na pwani ya Oman mapema jana Alhamisi kwa saa za eneo hilo.
Awali, kabla ya shambulizi hilo, Trump alisema Marekani na Iran zilikaribia kufikia makubaliano ya amani.
Mustakabali wa makubaliano hayo kwa sasa haujulikani kufuatia matukio ya hivi karibuni.