Makala ya 23 ya kipute cha Kombe la Dunia yataanza kutifua vumbi Alhamisi hii, Juni 11, katika mataifa ya matatu ya Marekani, Canada na Mexico.
Timu 48 zinashiriki kwa mara kwanza mwaka huu ikiwa ongezeko kutoka 32 za awali.
Hata hivyo, timu nane pekee zimenyakua kombe hilo katika makala 22 yaliyopita.
Samba Boys kutoka Brazil ambao wanajivunia kushiriki fainali zote wanasalia kuwa timu iliyo na ufanisi mkubwa wakitwaa mataji matano.
Brazil walishinda kombe hilo mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.
Ujerumani wameshinda Kombe la Dunia mara nne; 1954, 1974, 1990 na 2004.
The Azzuri ya Italia ambao walikosa kufuzu mwaka huu pia wanajivunia mataji manne;1934,1938,1982 na 1986.
Mabingwa watetezi Argentina wana mataji matatu kwa jina lao;1978,1986 na 2022.
Ufaransa wanayo mataji mawili wakiyanyakua mwaka 1938 na 1998, huku pia Uruguay ikiwa na vikombe viwili mwaka 1930 na 1950.
Uingereza walinyakua kombe hilo mwaka 1966 wakati Uhispania wakilinyakua mwaka 2010.