Kipkemboi na Kemuma washinda Nairobi Marathon

Kemuma alishinda mbio za wanawake kwa muda wa saa 2 dakika 27 na sekunde 46 mbele ya Jacinta Chepkoech na Nancy Jepleting waliochukua nafasi za pili na tatu mtawalia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Enock Kipkemboi na Joy Kemuma ndio mabingwa wa makala ya tano ya mbio za Nairobi City Marathon zilizoandaliwa Jumapili.

Kipkemboi ametumia saa 2 dakika 9 na sekunde 33 kukata utepe, akiafuatwa na Robert Kwambai kwa saa 2 dakika 9 na sekunde 51, huku Shadrack Kenduiywo akimaliza wa tatu kwa saa 2 dakika 9 na sekunde 56.

Kemuma alishinda mbio za wanawake kwa muda wa saa 2 dakika 27 na sekunde 46 mbele ya Jacinta Chepkoech na Nancy Jepleting waliochukua nafasi za pili na tatu mtawalia.

Brian Kogo na Doreen Kibet waliibuka washindi wa mbio za nusu marathon kwa wanaume na wanawake.

Zacharia Gacugu na Sharon Jepchirchir walishinda mbio za kilomita 10 kwa wanaume na wanawake.

Washindi wa marathon walituzwa shilingi milioni 3.5 kila mmoja.

Mbio hizo zilizokuwa na washiriki zaidi ya 17,0000, zilianzishwa na Waziri wa Michezo Salim Mvurya.

Share This Article