Rais William Ruto mapema Jumatano katika Ikulu ya Nairobi, amepokea stakabadhi za Mabalozi, walioteuliwa kuwakilisha mataifa yao humu nchini.
Akihutubu baada ya hafla hiyo Ruto aliahidi kuimarisha ushirikiano wa Kenya, na mataifa hayo na kushirikiana kwa pamoja kwa manufaa ya raia wa mataifa yao na Kenya.
Mabalozi hao ni pampja na Luis Fernando Carranza Cifuentes wa Guatemala, Salome Zulu Mmola wa Afrika Kusini, Anas Talib Ali Marafi wa Kuwait,na Olivia Charlotte Owen kutpka New Zealand.