Safari ya Kariobangi Sharks ligini yafika tamati

Dismas Otuke
1 Min Read

Safari ya miaka kumi ya klabu ya Kariobangi Sharks, kushiriki Ligi Kuu ya Kenya imetamatika ghafla siku ya Jumapili, baada ya kushushwa ngazi.

Sharks ambao walikuwa katika nafasi ya  16 wameishinda Sofapaka FC mabao 6-0, katika mechi ya kufunga msimu Jumapili ila wakashuka baada ya wapinzani wa karibu Ulinzi Stars na Mathare United kupata ushindi pia.

Sharks wanajiunga na Bidco United na Sofapaka kushuka hadi ligi ya daraja ya pili NSL msimu ujao.

 

Share This Article