Zaidi ya watu 300 walikamatwa mjini Paris,Ufaransa,Jumamosi usiku wakisherehekea ushindi wa klabu ya PSG, kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kuishinda Arsenal kupitia penati.
Polisi walisema takriban 416 walikamatwa katika miji mbalimbali ya Ufaransa ,baada ya sherehe hizo kugeuka na kuwa vurumai.
PSG walihifadhi kombe hilo baada ya kuwashinda mabingwa wa Uingereza,Arsenal mabao 4-3 kupitia penati baada ya sare ya bao moja ndani ya dakika 120.