Tanzania watamenyana na Senegal kwenye fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mabarubaru wasiozidi umri wa miaka 17 nchini Morocco Juni 2.
Senegal walijikatia tiketi kwa fainali baada ya kuwatema nje mabingwa watetezi na wenyeji Morocco kwa penalti 7-6, kufuatia sare ya bao moja katika nusu fainali ya pili Alhamisi usiku.
Upande wao, Serengeti Boys kutoka Tanzania walifuzu kwa fainali ya Afrika kwa wanaume kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Misri, kufuatia sare kappa ndani ya dakika 90.

Morocco watarejea uwanjani dhidi ya Misri katika mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne Juni Mosi.
Matifa 10 ya Tanzania, Senegal, Morocco, Misri, Msumbiji, Uganda, Algeria, Mali, Cameroon na Ivory Coast yamefuzu kucheza Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar.