John Mwandi ateuliwa Kasisi mpya wa Dayosisi ya Kitui ya kanisa Katoliki

Hadi uteuzi wake, Kasisi Mwandi alikuwa Naibu wa Kasisi Joseph Mwongela ambaye amehamishiwa Dayosisi ya Machakos.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kasisi John Mwandi ateuliwa Kasisi wa dayosisi ya Kitui ya Kanisa katoliki.

Papa Leo XIV amemteua Kasisi  John Mwandi kuwa  kuongoza dayosisi ya Kitui ya kanisa Katoliki.

Hadi uteuzi wake, Kasisi Mwandi alikuwa Naibu wa Kasisi Joseph Mwongela, ambaye amehamishwia Dayosisi ya Machakos.

Kasisi Mwongela anatarajiwa kuchukua mahali pa Kasisi wa sasa Norman King’oo ambaye muda wake wa kustaafu unakaribia.

Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, yalitangaza uteuzi wa Kasisi Mwandi katika hatua ambayo imepongezwa na waumini wa kanisa na viongozi wa kidini katika eneo hilo.

Akizungumza baada ya uteuzi wake, Kasisi Mwandi alielezea furaha yake huku akiahidi kuimarisha dayosisi hiyo na kupigia debe umoja miongoni mwa jamii ya waumini Wakatoliki.

Share This Article