Idadi ya ndovu nchini Msumbiji imepanda kwa asilimia 58 kutoka 9114 hadi 21,700,katika takwimu za kipindi cha miaka saba hadi kufikia mwaka 2025.
Waziri wa Kilimo Roberto Albino, amesema idadi hiyo imeongezeka kutokana na juhudi zilizowekwa na idara ya wanyamapori za kuwatafuta na kuwarejesha tembo waliokuwa wametoweka.
Waziri Albino alisema hayo alipoongoza maadhimisho ya miaka 15 ya uhifadhi wanyamapori.
Idadi hiyoi inafuatia hesabu za wanyamapori zilizofanywa mwaka jana huku idadi hiyo ya 21,700, ikiwa maradufu ya idadi ya tembo waliokuwa nchini Msumbiji mwaka 2018.
Aliongeza kuwa ufanisi huo umechangiwa pakubwa na sheria kali zilizowekwa na serikali kuzuia uwindaji haramu na kushirikisha jamii katika uhifadhi wanyamapori.
Kenya kwa sasa ina takriban ndovu 42,000, katika hifadhi mbalimbali za wanyama.