Serikali ya Congo imetengaza kuondoa hitaji la viza ya usafiri kwa wageni wote wanaotokea barani Afrika, kuanzia Januari mosi mwaka 2027 ili kurahisisha usafiri.
Kulingana na Rais Denis Sassou Nguesso, hatua hiyo itaongeza utangamano wa kikanda na kuhuisha biashara.
Hali hiyo itafanywa kuwa rahisi kwa watalii na wageni wa kutoka barani Afrika wanaonuia kuzuru Congo, aidha kwa biashara au kitalii.
Congo ni ya hivi punde kuondoa viza kwa wageni ikijiunga na Kenya, Rwanda, Ushelisheli na Togo.
Umoja wa Afrika unapendekeza kuondolewa kwa viza kwa wageni wa Afrika wanaozuru mataifa mengine barani ifikiapo mwaka 2063, ili kurahisisha biashara na matembezi kutoka mpaka hadi mwingine.