Rais Ruto awatakia Waislamu heri njema wanapoadhimisha Eid ul Adha

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto ametuma ujumbe wa heri njema  kwa jamii ya Waislamu nchini Kenya, wanapojiunga na wenzao kote duniani kuadhimisha  Eid ul-Adha.

Kupitia kwa taarifa, kiongozi wa taifa alisema kuwa maadhimisho ya Eid ul Adha ni msimu takatifu unaoashiria maadili ya imani, utiifu na kujitolea.

“Nawatakia heri njema na maadhimisho yenye amani na furaha,” alisema Rais Ruto.

Alitoa wito kwa wakenya kuwakumbuka wasiobahatika katika jamii, kuboresha umoja wa taifa na kujitolea kuishi kwa amani na utangamano, huku akiwatakia wote wanaosherehekea siku hii takatifu furaha, afya njema na baraka tele.

Eid-ul-Adha,ndiyo sherehe muhimu zaid katika likizo za kiislamu ambayo huadhimishwa kwa maombi ya waislamu kote duniani. Eid-ul-Adha inawahitaji waislamu kuabudu, kusherehekea na kutoa msaada.

Inaashiria hatua ya nabii Ibrahim ya kumtoa mwanawe kama sadaka kwa heshima ya mwenyezi Mungu.

Share This Article