Rais Ruto aongoza kikao cha Afrika kuhusu mageuzi ya taasisi

Rais alisema, kuwa na taasisi bora kunahitaji kubuni mifumo ya uongozi ya kujitegemea ili kuwezesha bara hili kuafikia ruwaza yake kwa raia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesisitiza haja ya Afrika kubuni taasisi dhabiti kupitia kwa utoaji wa pesa za kutosha na upatikanaji wa raslimali za kutosha, ili kuafikia utekelzaji wa Ajenda ya mwaka 2063.

Rais amesema haya jumanne alipoongoza kupitia mtandaoni kikao cha nne cha kamati ya usimamizi wa taasisi za Muungano wa Afrika .

Alitaja kuwa sera ya mabadiliko ni muhimu kwa mataifa ya Afrika, kutokana na kubadilika kila wakati kwa mifumo ya kisiasa.

Rais alisema, kuwa na taasisi bora kunahitaji kubuni mifumo ya uongozi ya kujitegemea ili kuwezesha bara hili kuafikia ruwaza yake kwa raia.

Share This Article