Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Hussein Mohammed amepongeza hatua ya shirikisho la soka duniani FIFA, kutupilia mbali mapendekezo ya baadhi ya wanachama wa kamati kuu ya kumpiga marufuku kwa madai ya ufisadi.
Akizungumza na Wanahabari leo baada ya kukutana na maafisa wa timu zote 18 ,zinazoshiriki ligi kuu nchini Kenya, Mohammed pia amewataka wapinzani wake kuweka kando maslahi yao na kufanya kazi pamoja.
Aidha,Mohamed amekariri kuwa shirikisho hilo litaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchini zile za CAF na FIFA, kuhakikisha shughuli zote za soka zinaendelea kama kawaida.
Kwenya barua yake kwa FKF,FIFA, ilikataa pendekezo la baadhi ya wanachama wa kamati kuu ya FKF, ya kumpiga marufuku Hussein Mohamed .