IGAD yamteua Rania Mustafa kuwa kaimu kiongozi wa ujumbe Sudan

Tom Mathinji
1 Min Read
Rania Mustafa ateuliwa kaimu kiongozi wa ujumbe nchini Sudan.

Shirika la kimaendeleo la IGAD, limemteua Rania Mustafa Hassan kuwa kaimu kiongozi wa ujumbe wa Sudan.

IGAD imesema hii ni hatua muhimu ya kurejelewa upya kwa ushirikiano kati ya IGAD na taifa hilo, na pia mpango wa kufungua upya afisi za IGAD Jijini Khartoum.

Kupitia kwa taarifa, IGAD imesema hatua ya kumteua kaimu kiongozi wa ujumbe nchini Sudan, ni sehemu ya mkakati wa ufunguzi wa afisi zake katika taifa hilo.

Kulingana na IGAD, uteuzi huo unaashiria mshikamano na watu wa Sudan na kujitolea kwake kwa uhusiano wa kidiplomasia katika kufanikisha upatikanaji wa amani, usalama na udhabiti.

Share This Article