Wanariadha wa Kenya warejea kutoka Ghana

Washindi wa dhahabu za Kenya walikuwa; Julius Yego katika urushaji Sagai,Edwin Too katika Decathlon,Kevin Chesang na Diana Wanza katika mita 10,000,Kelvin Loti katika mita 800, na Diana Chepkemoi katika mita 3,000. kuruka viunzi na maji.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kikosi cha mwisho cha timu ya Kenya iliyomaliza ya pili kwenye mashindano ya Riadha barani Afrika, kimewasili nchini mapema leo Jumanne kutoka Accra, Ghana.

Timu hiyo iliyokuwa na wanariadha 74, ilimaliza ya pili nyuma ya Afrika Kusini, kwa nishani sita za dhahabu, fedha tano na shaba saba.

Washindi wa dhahabu za Kenya walikuwa: Julius Yego katika urushaji sagai, Edwin Too katika Decathlon, Kevin Chesang na Diana Wanza katika mita 10,000, Kelvin Loti katika mita 800, na Diana Chepkemoi, katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Afrika Kusini ilihifadhi taji la jumla kwa nishani 22, dhahabu 9 fedha 3 na shaba 10, huku Ethiopia ikiibuka katika nafasi ya tatu kwa nishani 14 (dhahabu 5, fedha 4 na shaba 5).

Kenya sasa inaangazia michezo ya Jumuiya ya Madola itakayoandaliwa Scotland baina ya Julai 23 na Agosti 2 mwaka huu.

Share This Article