Ivory Coast yataja kikosi cha Kombe la Dunia

Mshambulizi wa Inter Milan Ange Yoan Bonny amejumuishwa kikosini huku wakijiandaa kurejea Kombe la Dunia mwaka huu wakirushwa kundi E pamoja na Ecuador,Ujerumani na limbukeni Curaçao.

Dismas Otuke
2 Min Read

Ivory Coast imetaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia kati ya Juni 12 na Julai 19 mwaka huu katika mataifa ya Mexico,Canada na Marekani.

Kocha Emerse Fae alitangaza kikosi chenye uzoevu pamoja na chipukizi wengi wao wakishiriki fainali za AFCON katika makala ya mwaka jana na yale ya mwaka 2023 wakiwa wenyeji.

Mshambulizi wa Inter Milan Ange Yoan Bonny, amejumuishwa kikosini huku wakijiandaa kurejea Kombe la Dunia mwaka huu wakirushwa kundi E pamoja na Ecuador,Ujerumani na limbukeni Curaçao.

Mshambulizi Nicolas Pépé,zamani akiichezea Arsenal na kwa sasa akiwa na Villarreal, ameitwa timuni baada ya kauchwa nje kwa AFCON mwaka jana .

Hata hivyo mshambulizi wa Charlotte FC Wilfried Zaha, ameachwa nje baada ya kushiriki AFCON, mwaka jana sawa na beki wa Nottingham Forest Willy Boly anayeuguza jeraha.

Makipa: Yahia Fofana (Rizespor), Mohamed Kone (Charleroi), Alban Lafont (Panathinaikos)

Mabeki: Emmanuel Agbadou (Wolverhampton Wanderers), Clement Akpa (AJ Auxerre), Ousmane Diomande (Sporting), Guela Doue (Racing Strasbourg), Ghislain Konan (Gil Vicente), Odilon Kossonou (Atalanta), Evan Ndicka (AS Roma), Wilfried Singo (Galatasaray)

Viungo:: Seko Fofana (Stade Rennais), Parfait Guiagon (Charleroi), Franck Kessie (Al Ahli), Christ Oulai (Trabzonspor), Ibrahim Sangare (Nottingham Forest), Jean-Michael Seri (NK Maribor)

Washambulizi: Simon Adingra (AS Monaco), Ange-Yoan Bonny (Inter Milan), Amad Diallo (Manchester United), Oumar Diakite (Cercle Brugge), Yan Diomande (RB Leipzig), Evann Guessand (Aston Villa), Nicolas Pepe (Villarreal), Bazoumana Toure (Hoffenheim), Elye Wahi (Nice)

Share This Article