Wenye magari ya usafiri wa umma wametangaza kuongeza nauli kwa asilimia 50, kufuatia kupandishwa kwa bei ya mafuta ya Petroli na Dizeli.
Wamiliki wa Matatu wametangaza kuwa bei hiyo mpya itaanza kutekelezwa Jumatatu ijayo Mei 18, ili kukidhia ongezeko la bei ya mafuta iliyotangazwa Alhamisi.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki matatu nchini
Albert Karakacha, ametaja kuwa ongezeko la bei ya mafuta iliyotangazwa na mamlaka ya kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta ya Petroli nchini (EPRA), kumeongeza gharama ya kuendesha biashara na hawana budi kupandisha nauli.
EPRA iliongeza bei ya Dizeli kwa shilingi 46 na senti 29, huku Petroli ikiongezeka kwa shilingi 16 na senti 65, kwa kila lita moja.
Lita moja ya Dizeli inauzwa kwa shilingi 242 na senti 92, wakati lita moja y Petroli, ikiuzwa Kwa shilingi 214 na senti 25 katika kaunti ya Nairobi.