Klabu ya Al Hilal Omdurman, kutoka Sudan, ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Rwanda, msimu wa mwaka 2025/2026.
Al Hilal walirejea nyumbani Khartoum, mapema wiki hii baada ya kunyakua taji ya Ligi kuu Rwanda, kuanza maandalizi kwa Ligi ya Mabingwa Afrika,msimu ujao.
Klabu hiyo ilizuru uwanja wa Hilal, ambapo itacheza mechi kadhaa za Ligi ndogo zitakazoiwezesha kushiriki Ligi ya mabingwa msimu ujao.
Omdurman wamezoa alama 73 kutokana na mechi 31, ikisalia michuano mitatu kukamilisha msimu wa Ligi Kuu Rwanda.