Chesang ashinda dhahabu ya kwanza ya Kenya,Ghana

Kenya ina medali nne kufikia sasa;dhahabu moja fedha 1 na shaba 2, huku mashindano hayo yakiingia siku ya nne leo Alhamisi Mei 14.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kevin Chesang alishinda dhahabu ya kwanza ya Kenya, katika Makala ya 24 ya mashindano ya Riadha Afrika Jumatano usiku, jijini Accra,Ghana.

Chesang ,alinyakua dhahabu ya mita 10,000 jana usiku katika siku ya pili ya mashindano ,ikiwa dhahabu ya kwanza kwa Kenya ya mbio hizo tangu mwaka 2012 mjini Porto Novo,Benin.

Chesang aliye na umri w miaka 20,aliibuka mshindi kwa dakika 28 sekunde 30.44.

Hagos Gared wa Ethiopia, ilinyakua nishani za fedha huku Silas Senchura wa Kenya, akiridhia shaba.

Edwin Too baada ya kupokea medali ya fedha ya Decathlon

Awali jana Edwin Too, alishinda fedha katika shindano la Decathlon, akiboresha shaba aliyoshinda mwaka 2024 nchini Cameron.

Kenya ilifunga siku ya pili kwa medali ya shaba ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti jinsia mchanyato.

Timu ya Kenya baada ya kushinda shaba ya mita 400 kwa wanariadha wanne mseto

Kenya ina medali nne kufikia sasa;dhahabu moja fedha 1 na shaba 2, huku mashindano hayo yakiingia siku ya nne leo Alhamisi Mei 14.

Fainali za Wakenya ni pamoja na mita 800 kwa wanume na wanawake na mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Share This Article