Rais Museveni kuapishwa Jumanne kwa muhula wa saba

Tom Mathinji
1 Min Read
Museveni ameidinishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Januari 12 mwaka ujao / Picha kwa hisani ya Reuters

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne kwa muhula wa saba, kwenye sherehe itakayoandaliwa katika uwanja wa Kololo, Jijini Kampala.

Zaidi ya Marais na Viongozi Wakuu 50 wa serikali watahudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa rais huyo, aliyeibuka mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu ulioandaliwa Januari 15, 2026.

Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, ni miongoni mwa wageni wanaohudhuria sherehe hiyo, wengine wakiwa ni pamoja na Rais wa Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hassan Sheikh Mahamud wa Somalia, Atske Selassi wa Ethiopia, Salva Kiir wa Sudan Kusini miongoni mwa wengine.

Jumatatu jioni Rais Museveni aliwaandalia dhifa ya jioni wageni wake katika Ikulu ya Entebe, huku akishiriki mazungumzo ya faragha na mwakilishi wa Rais Donald Trump wa Marekani Nick Checker.

Hali ya usalama imeimarishwa, huku miundombinu ikiboreshwa tayari kwa sherehe hiyo,

Share This Article