Barcelona wanyakua ubingwa wa La Liga kwa mara ya 29

Marcus Rashford aliwaweka wenyeji Barca, kifua mbele ugani Nou Camp kunako dakika ya 9, kabla ya Ferran Torres, kuongeza la pili dakika ya 18.

Dismas Otuke
1 Min Read

FC Barcelona, walinyakua ubingwa wa ligi Kuu nchini Uhispania almaarufu La Liga, kwa mara ya 29 Jumapili usiku, baada ya kuwacharaza mahasimu wa jadi Real Madrid mabao 2-0.

Marcus Rashford aliwaweka wenyeji Barca, kifua mbele ugani Nou Camp, kunako dakika ya 9, kabla ya Ferran Torres, kuongeza la pili dakika ya 18.

Katalunya chini ya kocha Hansi Flick, walihifadhi taji hiyo ya Ligi Kuu wakizoa jumla ya pointi 91, baada ya mechi 35 .

Madrid ambao wamekuwa na msimu mbovu wanafuata kwa umbali kwa alama 77, wakati Villareal ikishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 69.

Girona,Deportivo Alaves,Levante na Real Oviedo, zinakabiliwa na hatari ya kuenguliwa ligini zikiambatana katika nafasi za 17,18,19 na 20 mtawalia.

Share This Article