Wanariadha wa Kenya wajiandaa kwa mashindano ya Afrika,Accra

Kenya inawakilishwa na kikosi cha wanariadha 74, wanaoshiriki katika mashindano ya mbio na yale ya ndani ya uwanja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa Kenya walifanya mazoezi ya kwanza Jumapili jioni katika chuo kikuu cha Accra nchini Ghana, tayari kwa makala ya 24 ya mashindano ya riadha barani Afrika.

Mashindano hayo yataanza kesho Jumanne na kukamilika Jumapili Mei 17.

Kenya inawakilishwa na kikosi cha wanariadha 74, wanaoshiriki katika mashindano ya mbio na yale ya ndani ya uwanja.

Katika makala ya mwaka 2024 mjini Doula,Cameroon ,Kenya ilimaliza ya pili nyuma ya Afrika Kusini, kwa medali 19,dhahabu 5 fedha 7 na shaba 7.

Share This Article