Kampuni ya kutengeza vifaa vya michezo ya Marekani,Nike, imefungua duka la kwanza nchini Kenya katika eneo la Sarit Centre.
Hafla hiyo ikiandaliwa Jumatano na kuhudhuriwa na maafisa wa Nike maafisa Wa chama cha Riadha Kenya, pamoja na bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge.
Kampuni ya Nike hutengeza sare na viatu ambavyo hutumia na wanariadha wa Kenya katika mashindano ya kimataifa.
Duka hilo litakuwa likiuza mavazi ya michezo.