Rais Ruto awasili Tanzania kwa ziara ya kiserikali

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto wa Kenya amewasili jijini Dar es Salaam,Tanzania, Jumatatu adhuhuri kwa ziara rasmi ya kiresikali.

Rais alilakiwa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan, punde alipowasili.

Ruto alipata fursa ya kukagua gwaride liloandaliwa kwa heshima yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia bunge la kitaifa la Tanzania kesho kando na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake.

Share This Article