Derby ya Kariakoo ya 196 kati ya watani jembe Simba na Yanga imemalizikia sare ya mabao 2 Jumapili jioni katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, kisiwani Zanzibar.
Libase Gueye alipachika goli la kwanza kwa wenyeji Simba dakika ya tatu ya mchezo naye Clatous Chama atanua uongozi kwa bao la pili dakika ya 10.
Yanga walijibu goli moja kunako dakiak ya 17 kupitia kwa Prince Dube, kisha wakasawazisha dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Bakari Mwamnyeto.
Matokeo hayo yameiacha Yanga kileleni kwa poinyi 48, baada ya mechi 20 zikisalia 10 msimu ukamilike ,alama 5 zaidi ya Simba walio katika nafasi ya pili.