Timu ya Kenya ya mita 400 mseto yafuzu kwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya wanariadha wanne kupokezana kijiti mseto imejikatia tiketi kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao baada ya kumaliza ya pili katika mchujo wa Mbio za Dunia za kupokezana kijiti mjini Gaberone,Botswana.

George Mutinda,Mercy Oketch,Kelvin Tonui, na Mercy Chebet, walimaliza katika nafasi ya pili wakiweka rekodi mopya ya Afrika ya dakika 3 sekunde 9.87.

Mchujo huo wa tatu umeshindwa na Uingereza, kwa dakika 3 sekunde 9.69, huku timu zote mbili zikiwahi tiketi ya mashindano ya Dunia mwaka ujao.

Italia imemaliza ya tatu.

Kenya inawakilishwa na timu tano kwenye mbio za dunia zinazoandaliwa kwa mara ya kwanza Afrika.

Share This Article