Huduma ya Taifa ya Polisi nchini Kenya imesema watu 10 wamefariki kutokana na mafuriko, wakati huu wa masimu wa mvua kubwa inayoshuhudiwa kote nchini humo.
Kulingana na Huduma hiyo, eneo la Mashariki mwa Kenya ndilo limeathirika zaidi huku watu 7 miongoni mwa waliofariki wakitoka eneo hilo.
Taarifa hiyo ya Polisi kwenye ukurasa wa X, ilisema madaraja mawili, daraja la Mwena kaunti ya Kwale na daraja la Ngomeni kaunti ya Kitui, na kutatiza shughuli za uchukuzi.
“Maporomoko ya ardhi pia yameripotiwa katika kaunti ndogo ya Tambach, Elgeyo Marakwet, na kuhatarisha maisha ya wakazi na miundombinu,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi.
Aidha, kupitia kwa taarifa hiyo makundi ya dharura yanatekeleza shughuli za uokoaji, na kurejesha huduma muhimu.
” Tunawahimiza wananchi hasaa walio katika maeneo yaliyoathirika kuwa waangalifu, kuepuka mafuriko na kuzingatia ushauri kutoka kwa maafisa wa utawala,” ilisema taarifa hiyo ya polisi.