Ketraco kuilipa kampuni ya ufaransa shilingi milioni 220

Dismas Otuke
0 Min Read

Mahakama kuu ya Kenya imeamrisha kampuni ya serikali ya usambazaji kawi ya Ketraco, kulipia kampuni ya Ufaransa shilingi milioni 220, kutokana na mradi uliokwama wa nishati ya upepo wa Loiyangalani-Suswa.

Pia mahakama hiyo ilipuuzilia mbali ombi la kampuni hiyo ya Enterprise Generale Malta Forests, la kutaka fidia ya shilingi milioni 500, kwa kupotezewa muda baada ya kushindwa kuthithibitisha.

TAGGED:
Share This Article