Aprili 29 mwaka 2026, ilikuwa ya kihistoria baada ya serikali ya Morocco, kusaini ushirikiano na sekta ya kibinafsi, hatua itakayowezesha upatikanaji wa huduma za maji kwa raia wote nchini humo.
Wizara ya maji na mitambo kwa ushirikiano na wizara ya viwanda,pamoja na sekta ya kibinafsi zimesaini makubaliano ya kujenga miradi ya maji kufuatia agizo la Mfalme Mohammed wa sita .
Waziri wa maji Nizar Baraka,amesema makubaliano hayo yataleta usawa wa ugavi miundo mbinu ya usambazaji na usimamizi wa maji.

Mwafaka huo pia utashuhudia uwezeshaji wa wataalam wa sekta za maji na viwanda kupitia kwa utoaji mafunzo ya kiufundi, ili kuwapa fursa dhid ya wenzao kutoka barani Afrika.