Wabunge wa kutoka maeneo ya Kaskazini wameitaka serikali kuchukua hatua za dharura kumaliza mapigano yanayoendelea katika mpaka wa Mwingi na Garissa.
Wabunge hao wamesikitishwa na hali ilivyo kwa sasa huku wakitoa rambirambi kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao kwenye vurumai hizo.
Aidha, wametaja kuwa kuendelea kwa mapigano hayo kutasambaratisha uhusiano wa karibu na wa muda mrefu ambao umekuwa baina ya jamii za eneo hilo.
Wamesema haya siku ya Alhamisi, walipowahutubia wanahabari jijini Nairobi ,wakikashifu vita hivyo ambavyo vinazidi kusababisha vifo na uharibifu mkubwa.