Watu 518 waliuawa wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania Oktoba mwaka jana.
Tume ya Rais ya kuchunguza machafuko ya baada ya uchaguzi imefiuchua wakati ilianza vikao vya kuwahoji rai ana wadau mbalimbali kutokana na wanachofahamu kuhusu matukio hayo.
Kulingana na tume hiyo idadi ya vifo imethibitishwa kutokana na ripoti kutoka kwa hospitali za umma na zile za kibinafsi.
Hata hivyo tume hiyo imesema huenda kuna vifo ambavyo havikunakiliwa kutokana na aidha kutoripotiwa hospitali au katika vyombo vya kiusalama.
Rais Samia Suluhu Hassan,alibuni tume hiyo ili kutoa ripoti kamili kuhusu idadi ya wanaohitajika kulipwa ridhaa na pia kuleta maridhiano ya kitaifa.
Pia kumekuwa na shinikizo kutoka kwa umma na mashirika ya kijamii kuhusu yalioyojiri na idadi ya waliouawa na polisi katika machafuko hayo.