Hussein apumua,Mahakama yasitisha kufurushwa kwake FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la soka humu nchini FKF anayekabiliwa na utata Hussein Mohammed, amepata afueni siku ya Jumatatu, baada ya Jopo la kutatua migogoro michezoni kusitisha kwa muda kutimuliwa kwake afisini na kamati kuu- NEC.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 6 mwezi ujao.

Jopo hilo limesitisha utekelezaji wa maazimio yote yaliyoafikiwa kwenye kikao cha Ijumaa iliyopita hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Kamati ya NEC ya FKF iliwapiga marufuku Rais Hussein Mohamed na Katibu wake mkuu Dennis Gicheru Aprili 24,ili kupisha uchunguzi kuhusiana na madaiya  sakata ya ufisadi katika utoaji zabuni wa bima wakati wa  fainali za CHAN mwaka uliopita.

Share This Article