Mkenya Sabastian Sawe, aweka rekodi ya dunia ya Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkenya Sabastian Sawe ameandikisha rekodi  mpya ya Dunia katika mbio za marathon ya saa 1 dakika 59 na sekunde 35,akivunja rekodi ya marehemu Kelvin Kiptum ya saa 2 na sekunde 35, iliyoandikishwa mwaka 2023.

Sawe ameweka rekodi hiyo Jumapili alipohifadhi taji yake ya mwaka jana ya London Marathon .

Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 30, ndiye mwanaume wa  kwanza kukamilisha mbio za marathon chini ya saa 2.

Mwethiopia Yomif Kejelcha amemaliza wa pili kwa saa 1 dakika 59 na sekunde 41, huku Mganda Jacob Kiplimo akichukua nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2  na sekunde 28.

Amos Kipruto alichukua nafasi ya tatu huku Mkenya mwingine Geofrey Kamworor akiambulia nafasi ya nane.

Share This Article