Hellen Obiri amemaliza wa pili katika makala ya mwaka huu ya mbio za London marathon zilizoandaliwa Jumapili nchini Uingereza.
Obiri aliyekuwa akishiriki mbio hizo kwa mara ya kwanza amemaliza wa pili kwa muda wa saa 2 dakika 15 na sekunde 53 ,sekunde 2 mbele ya mwenzake na bingwa wa mwaka 2021 Joyceline Jepkosgei,aliyechukua nafasi ya tatu.
Tigist Assefa wa Ethiopia amehifadhi taji yake alipotwaa ubingwa kwa muda wa saa mbili dakika 15 na sekunde 41,akivunja rekodi yake ya Dunia kwa wanawake.