Uhaba wa maji:Jinsi Mfalme wa Morocco, Mohammed VI ametatua changomoto ya maji

Dismas Otuke
2 Min Read

Huku mataifa mengi ya Afrika yakikabiliwa na changamoto za kila siku za mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa maji ,serikali ya Morocco imebuni mradi na mpango wa kupigiwa mfano wa kumaliza ukosefu na uhaba wa maji.

Chini ya uongozi wa Mfalme Mohammed VI ,serikali ya Morocco inatumia mkakati unaoshirikisha mbinu nyingi ikiwemo uwekaji akiba kubwa ya maji,na miundombinu ya kisasa unaohakikisha kuwepo kwa maji toshelezi katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Morocco inatumia sera yake ya mabwawa ambayo imepigwa jeki na Mfalme Mohammed VI.

Hivi maajuzi akiba ya kitaifa ya maji nchini Morocco ilipita cubic meter bilioni 1.3, hatua inayoafiki uwekezaji maridhawa na wenye tija  chini ya Ruwaza ya Mfalme.

Ufanisi wa mradi huu ni dhihirisho la uwekezaji bora ambao ni nguzo muhimu katika kudhibiti mvua isiyotabirik nchini humo .

Mpango huu mahususi umechangia uwepo wa maji ya kutosha ya kunywa na pia kutumika kwa shughuli za kilimo ambazo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Morocco.

Kando na mabwawa Morocco imetafuta mbinu nyingine za dharura za kukidhi mahitaji ya maji kwa  raia wake  ikiwemo matumizi ya magari yanayotakasa maji  na kuondoa chumvi na madini na kisha kusafirisha nyumba hadi nyumba  ili kutumika na binadamu .

Kulingana na waziri wa maji nchini Morocco, Nizar Baraka, mipango ya matumizi ya magari kusafirisha na kutakasa maji inatumika sana katika maeneo yenye uhaba wa maji, ili kuhakikisha  upatikanaji wa maji ya matumizi kila wakati.

Ufanisi wa Morocco katika sekta ya maji hautegemei tu teknolojia bali kwa ruwaza ya kisiasa ya muda mrefu chini ya Mfalme Mohammed VI.

Mpango huo wa maji unajumuisha uhifadhi wa mazingira,matumizi yasiyo na uharibifu,na uwekezaji katika kawi safi.

 

Share This Article