Obiri,Sawe na Jepkosgei kutimka London Marathon kesho

Dismas Otuke
1 Min Read

Mathew Sawe atajitosa uwanjani Jumapili kutetea taji la mbio za London Marathon  nchini Uingereza kwa wanaume.

Sawe atakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Waganda Joshua Cheptegei na Jacob Kiplimo na wanariadha kutoka Ethiopia Tamirat Tola na  Yomif Kejelcha.

Mbio za wanawake zitawashirikisha Wakenya Hellen Obiri na Joyceline Jepkosgei watakaopambana  na bingwa mtetezi Tigst Assefa .

Mbio za London zitakuwa za tatu katika msururu wa mbio kuu ulimwenguni baada ya Tokyo Marathon mwezi jana na Boston Marathon Jumatatu wiki hii.

Share This Article