Bunge la Uganda lapitisha bajeti ya shilingi Trilioni 2.9

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunge la Uganda siku ya Ijumaa limeptisha bajeti ya serikali ya shilingi trilioni 84.3, za Uganda sawa na shilingi trilioni 2.93 za Kenya, kwa makadirio ya matumizi ya mwaka 2026/2027.

Kikao cha bunge cha kupitisha bajeti hiyo kilikabiliwa na pingamizi kali kutoka kwa Wabunge wa upinzani walioishutumu serikali kwa matumizi mabaya ya pesa.

Upande wa serikali uliitetea bajeti hiyo ukisema utachangia kwa ukuaji wa kiuchumi katika kipindi hicho cha matumizi.

Walimu,wahudumu wa afya,wanasayanzi na wafanyakazi wengine wa umma wanatarajiwa kupata nyongeza ya mishahara.

Bajeti hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini  Uganda, ikiongezeka kutoka kwa shilingi za Uganda 72.38 za bajeti ya mwaka mwaka 2025/2026.

 

 

Share This Article