Guterres apongeza kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres

Muda mfupi baada ya Iran kutangaza kufungua mlango bahari wa Hormuz ili kuruhusu meli kupita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amepongeza hatua hiyo akiitaja kuwa bora zaidi.

“Nakaribisha tangazo la Iran kwamba mlango bahari wa Hormuz umefunguliwa kwa meli za kibiashara wakati wa kipindi cha kusitisha vita. Hatua hiyo ni mkondo ufaao,” alisema Guterres kupitia kwa taarifa.

Alisema Umoja wa Mataifa unataka kurejeshwa kwa haki na uhuru wa mlango bahari wa Hormuz, ukiongeza kuwa eneo hilo linapaswa kuheshimiwa na kila mmoja.

“Ninatumai ya kwamba, usitishwaji wa vita pamoja na hatua hiyo, zitachangia kuimarisha mazungumzo yanayoendelea yanayoongozwa na Pakistan,” aliongeza Guterres.

Alisema anaunga mkono juhudi za kidiplomasia zinazolenga kumaliza mzozo Mashariki ya Kati.

Iran imetangaza kufungua mlango bahari wa Hormuz kwa meli za kibiashara, wakati wa kipindi cha siku kumi cha suitishaji vita dhidi ya Lebanon.

Share This Article