IEBC imewasajili wapiga kura wapya milioni 1.3

Tom Mathinji
1 Min Read
IEBC yawasajili wapiga kura wapya milioni 1.3.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imewasajili wapiga kura wapya 1,370,930 tangu zoezi endelevu la usajili wa wapiga kura lilipoanza  March 30, 2026.

Kupitia kwa taarifa Ijumaa, tume hiyo ilisema iliwasajili wapiga kura wapya 495,429 katika muda wa wiki moja tangu Aprili 9, 2026.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa usajili wa wapiga kura wapya, huku wakiwa 150,166 ikifuatwa na kaunti ya Kiambu ikinakili wapiga kura wapya 72,055 nayo Kakamega ikiwa ya tatu kwa kuwasajili wapiga kura wapya 61,797.

Nakuru na Machakos ziliwasajili wapiga kura wapya 57,068 na 47,348 mtawalia.

Tume hiyo imetaja usajili huo kuwa ishara ya kuwa na imani na mchakato wa demokrasia wa taifa hili, ikidokeza kuwa zoezi hilo limejumuisha maeneo yote, wakiwemo wazee kwenye maeneo ya ndani zaidi hapa nchini.

TAGGED:
Share This Article