Washukiwa wawili wa uhalifu wakamatwa Rongai

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wauhalifu wakamatwa Rongai.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika eneo la Kajiado Kaskazini, kaunti ya Kajiado, wamewatia nguvuni washukiwa wawili wa uhalifu na kupata bunduki ambayo ilikuwa imeibwa kutoka kwa afisa wa polisi.

Operesheni hiyo ya kijasusi, ililenga maeneo ya Kware na barabara ya Mandazi ambapo washukiwa hao walitiwa mbaroni.

Washukiwa waliokamatwa ni Cyrus Mureithi Mburu, mwenye umri wa miaka 54, na Peter Kangethe, mwenye umri wa miaka 49.

Baada ya maafisa hao kutekeleza msako kwenye nyumba ya washukiwa hao, walipata risasi 15, mafuta nusu lita ya bunduki.

Bastola hiyo iliyopatikana inaaminika kuibwa kutoka kwa afisa wa polisi kutoka kitengo cha majengo ya serikali.

Aidha bunduki mbili bandia, pingu, funguo na upanga pia zilipatikana kwenye operesheni hiyo.

TAGGED:
Share This Article