Marioo amtaka Nadia aseme ukweli kuhusu msanii wa Bongo aliyemsumbua

Msanii huyo alichelewa sana kufika katika eneo la kuandaa video ya wimbo wao wa pamoja.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Tanzania Marioo sasa anamtaka Nadia Mukami mwanamuziki wa Kenya, aseme ukweli kuhusu msanii wa Bongo aliyemsumbua.

Marioo analalamika akisema kwamba madai ya Nadia yamefanya jina lake lihusishwe, jambo ambalo amelikanusha vikali akieleza kuwa kwa upande wake walifanya kazi hiyo kwa ushirikiano mzuri bila changamoto yoyote.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, wengi wakitaka ukweli uwekwe wazi ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza.

Akizungumza katka mahojiano, Nadia alisimulia kuhusu ushirikiano iliokuwa mbaya zaidi katika maisha yake kama msanii ambapo alisema kwamba ni msanii kutoka Tanzania.

Nadia alisema alikubaliana na msanii husika kwamba asafiri na kundi lake hadi Tanzania kwa barabara wakatengeneze video ya wimbo wao wa pamoja.

Walipofika Tanzania, mawasiliano yao na msanii huyo yalikuwa ya tabu kwani alikuwa hapatikani kwenye simu. Yeye na wenzake waliendelea kuandaa eneo la kunakili video lakini msanii huyo hakuja hadi usiku.

Alipoulizwa iwapo kazi hiyo mwishowe ilitoka, Nadia alicheka akielezea kwamba meneja wa msanii huyo wa Bongo aliufungia hadi pale ambapo Nadia naye angehusishwa kwenye wimbo wa msanii huyo.

Wasanii ambao Nadia ameshirikiana nao kikazi kutoka Tanzania ni Marioo na Rayvanny ingawa hakutaja jina la aliyemkosea.

Share This Article