Waziri wa Fedha nchini Benin Romuald Wadagni, ameshinda Uchaguzi wa Urais nchini Benin, huku akipata zaidi ya asilimia 94 ya kura zilizopigwa.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Sacca Lafia, siku ya Jumatatu alitangaza kuwa matokeo hayo ni asilimia 90 ya kura zote zilizopigwa, akiongeza kuwa idadi ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo ni asilimia 58.78.
Mwaniaji wa Urais wa upinzani Paul Hounkpe, alikiri kushindwa kupitia kwa taarifa kwenye vyombo vya habari Jumatatu usiku.
“Kwa Romuald Wadagni, nakupongeza. Demokrasia inahitaji kuheshimiana na uwezo wa kuepuka tofauti za kisiasa,’ alisema Hounkpe kwenye taarifa yake ya kukubali kushindwa.
Wadagni anamrithi Patrice Talon ambaye anaondoka baada ya kuikamilisha mihula miwili ya miaka mitano kila muhula.